JAJI MKUU AWATAKA WATUMISHI WA MAHAKAMA KUELIMISHA WANANCHI JUU YA UTOAJI HAKI.

 Jaji mkuu Prof,Ibrahim Hamis Juma amefanya ziara Mkoa wa Tanga akianzia wilaya ya Pangani kujionea Hali ya majengo ya mahakama na kuona jinsi Utoaji wa haki kwa njia ya Tehama


Akizungumza akiwa Wilayani Pangani Jaji mkuu amesema lengo la ziara yake ni kuona hali ya Utoaji wa haki kwa wananchi ikoje na kuzungumza na wadau na kusikia changamoto zilizopo.

Pia Jaji mkuu amesema kwa wilaya Pangani tatizo kubwa lililopo ni ukusanyaji wa ushahidi kushindwa kufikia Kikomo kutokana ucheleweshaji wa ukusanyaji wa ushahidi bila kuleta mafanikio .

 "Kumekuwa na mlolongo mrefu wa Utoaji wa ushahidi hasa kwenye makosa ya madawa ya kulevya mashauri mengi yanakwama kutokana na kutokuwa na ufahamu kwa upande wa waendesha mashtaka hivyo ni wajibu wa kuwaelimisha kujua sheria.alisema Jaji mkuu"

Kwa upande wa kesi za mirathi Jaji Mkuu amesema kumekuwa na tatizo kwa watu wengi kutokuwa na ufahamu wa usimamizi wa mirathi na kuona kuwa mirathi ni kurithi mali na kutumia bila kufwata utaratibu na sheria.

" Wapo wananchi hawafahamu sheria na wanakuja mahakamani nakusema wao ni wasimamizi wa mirathi hivyo hata kama wamepata kibali Cha familia wanatakiwa kupewa elimu na kutenda haki kwa  wafiwa.alisema"

Jaji ametoa siku kumi na nne (14) kwa watumishi wa mahakama kuweka anuani za makazi katika ofisi zote za serikali na kutumia postcode katika Utoaji wa haki na katika shughuli mbalimbali za kimahakama

"Serikali inaendeleaa na zoezi Muhimu la postcode hivyo nasi watumishi wa mahakama tufanye kazi zetu kwa kutumia Postcode katika utoaji haki na uandikaji wa Barua kutumia anuani za makazi katika Barua zetu na taratibu zote za mahakama.alisema Jaji mkuu.





Comments